Gwiji wa soka raia wa Uingereza ambaye aliwai kufanya vyema na kucheza kwa mafanikio klabuni Chelsea, Frank Lampard ametoa sifa kwa nyota wa Chelsea, Willian Borges da Silva ambaye jana alikuwa akiiongoza Chelsea ilipopoteza dhidi ya Barcelona huko nchini Hispania na kutofanikiwa kucheza hatua ya robo fainali ya michuano hiyo.
"Willia alikuwa katikati ya kila jambo zuri ambalo Chelsea wameyafanya. Amekuwa kwenye kiwango bora kwa kila dakika. Bila ubishi Willian anaonyesha ana ubora wa kucheza timu yoyote duniani, hata Barcelona. Tumekuwa tukitoa sifa nyingi kwa Lionel Messi lakini nadhani hata Willian anaweza kucheza katika nafasi hiyo" alisema gwiji huyo ambaye kwa sasa anafanya kazi ya uchambuzi wa soka katika chombo cha BT Sport.
Willian amekuwa msingi imara kwa Chelsea haswa katika kipindi hiki ambacho safu ya ushambuliaji ya Chelsea inapoonekana kutetereka akiiongoza vyema katika kila mchezo anapopewa nafasi licha ya kuonekana haaminiki na kocha Antonio Conte. Nyota huyo mpaka sasa ameshaichezea Chelsea michezo 44 tu huku michezo ya ligi kuu akicheza 16 na kufanikiwa kufunga magoli 6 na kutengeneza mengine sita, hiyo ni kwa ligi kuu tu.
LAMPARD ATOA NENO JUU YA KIWANGO NA UBORA WA WILLIAN
Share This
Tags
# Chelsea FC
# Chelsea Habari
Share This
About Darajani 1905
Chelsea Habari
Labels:
Chelsea FC,
Chelsea Habari
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


No comments:
Post a Comment