Nyota wa zamani wa Chelsea, Diego Costa ambaye amejiunga na klabu ya Atletico Madrid kwa usajili wa kudumu katika dirisha la usajili la mwezi Januari kwa dau la paundi milioni 55 ametoa neno la kumkejeli kocha wa sasa wa Chelsea, Antonio Conte ambaye jana alikuwa uwanjani kuiongoza klabu ya Chelsea katika mchezo wa klabu bingwa barani Ulaya dhidi ya Barcelona.
Nyota huyo raia wa Hispania alituma ujumbe wa picha kupitia mtandao wa Instagram akionyesha kikosi cha Chelsea kilichoshuka uwanjani katika mchezo huo huku akiziba jina la kocha Antonio Conte kwa kutumia wino mweupe. Ujumbe huo ulizua zengwe na kujiuliza ni nini nyota huyo alikimaanisha kwa kutuma ujumbe huo.
Nyota huyo aliondoka Chelsea kwa ugomvi mkubwa ulioibuka kati yake na kocha huyo raia wa Italiano ambapo aligoma kuungana na Chelsea licha ya timu hiyo kuanza msimu mpya na hivyo kuamua kujiungana na Atletico Madrid, klabu yake ya zamani ambapo hakuruhisiwa kuichezea mchezo wowte wa kiushindani mpaka litakapofika dirisha dogo la usajili la mwezi Januari.
DIEGO COSTA AANZISHA UGOMVI NA KOCHA ANTONIO CONTE
Share This
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


No comments:
Post a Comment