EDEN HAZARD AMTETEA CARRASCO - Darajani 1905

EDEN HAZARD AMTETEA CARRASCO

Share This
Nyota wa Chelsea, Eden Hazard amemtetea nyota mwenzake raia wa Ubelgiji, Yannick Carrasco aliyejiunga na klabu mojawapo ya nchini China inayoshiriki ligi kuu nchini humo. Carrasco aliyekuwa anaichezea klabu ya Atletico Madrid ya nchini Hispania amejiunga na klabu hiyo ya nchini China kabla ya kuanza kwa msimu mwengine wa ligi kuu nchini humo ambayo imeanza mwezi wa pili mwaka huu.

"Sijui ni kipi alikiwaza kujiunga na klabu hiyo maana sipo kichwani mwake, lakini najua kuna kitu cha maana alikilenga mpaka kuamua kwenda huko. Nafikiri China ndilo lilikuwa chaguo la mwisho kwake na lililobaki maana kama angeendelea kusalia Atletico huenda asingepata nafasi ya kucheza mpaka mwishoni mwa msimu"

"Akiwa China atapata nafasi nzuri ya kucheza na kuonyesha uwezo wake, kiukweli, ni heri ukaenda China unapokuwa na uhakika wa kupata nafasi, kuliko kubaki Hispania ambapo unakaa benchi. Kwenda kule ni kama uamuzi mbaya kama wengi wanavyofikiri, lakini naamini mwenyewe ana sababu zilizomfanya aende uko" alisema nyota huyo.

Yannick Carrasco aliwai kutajwa kutakiwa na klabu ya Chelsea haswa katika dirisha dogo lililopita ambapo mchezaji huyo alikuwa na maelewano mabaya na wachezaji na baadhi ya watu wa benchi la ufundi klabuni Atletico Madrid mpaka ikadaiwa kocha wake Diego Simeone aliwaambia viongozi wa klabu kwamba mchezaji huyo auzwe haraka.

No comments:

Post a Comment