LIKITOKEA HILI, BASI DAVID LUIZ ATABAKI CHELSEA - Darajani 1905

LIKITOKEA HILI, BASI DAVID LUIZ ATABAKI CHELSEA

Share This
Mashabiki wengi wa Chelsea wamekuwa wakihoji juu ya hatma ya nyota wa klabu hiyo, David Luiz ambaye anaonekana kupoteza nafasi yake ya kikosi cha kwanza huku kinda Andreas Christensen akionekana kuaminika zaidi na kocha Antonio Conte huku David Luiz aliyeisaidia kushinda taji la ligi kuu msimu uliopita akicheza michezo 17 tu msimu huu.

Mara baada ya hilo kutokea huku ikihisiwa huenda kuna ugomvi kati ya kocha huyo pamoja na mlinzi huyo raia wa Brazil ambapo baadae kocha Antonio Conte alikana na kusema hakuna chochote kibaya kinachoendelea baina ya wawili hao.

Sasa kuna taarifa zinahisiwa kuendelea klabuni hapo ambapo zinadai David Luiz ataendelea kusalia kuwa mchezaji wa Chelsea kama tu kocha Antonio Conte ataondoka klabuni hapo na kuja kocha mwengine.

No comments:

Post a Comment