JOHN TERRY NA FRANK LAMPARD KUMRITHI ANTONIO CONTE? - Darajani 1905

JOHN TERRY NA FRANK LAMPARD KUMRITHI ANTONIO CONTE?

Share This
Moja kati ya mambo waliyoyaongea magwiji wa soka Frank Lampard na John Terry pindi walipokuwa wakiwaaga mashabiki wa Chelsea katika vipindi tofauti walikuwa wakisema ipo siku watarudi Chelsea na kutoa asante yao kwa vitendo au kwa kutumika vingine. Kutumika huko kulitafsiriwa kwamba walitaka kuwa makocha wa Chelsea siku moja au kuwa katika benchi la ufundi.

Na sasa huenda maneno yao yakakamilika mapema kuanzia sasa, huenda mmojawapo au wote kwa pamoja watajumuishwa kwenye benchi la ufundi la Chelsea. Ndio, hiyo ni mara baada ya wakongwe hao kuonekana wakifika Chelsea na kuwa na kikao kifupi na kiongozi wa bodi ya Chelsea ambaye anashuhurika na mambo yote ya usajili na kukuza vijana katika akademi ya Chelsea, mwanamama Marina Glanovskaia.

Nyota hao wamekuwa na kikao hicho na mwanamama huyo huku ikitajwa huenda yalikuwa ni mzungumzo ili wakongwe hao wafike klabuni Chelsea na kujiunga na benchi la ufundi klabuni hapo.

John Terry kwa sasa ni mchezaji na nahodha wa klabu ya Aston Villa na amekuwa akishirikiana vyema na kocha wa klabu hiyo Steve Bruce katika kuiendesha klabu hiyo mpaka kufikia sasa ambapo klabu hiyo inapambana kurudi katika ligi kuu Uingereza ambapo inashiriki ligi daraja la kwanza la Uingereza maarufu kama Championship wakati kwa upande wa Frank Lampard anakaribia kupokea leseni ya daraja A la ukocha huku kwa sasa akiwa hajafudhu kupata leseni itakayomruhusu kuiendesha timu na kushiriki michuano ya barani Ulaya ikiwemo michuano ya klabu bingwa baranai Ulaya maarufu kama UEFa Champions League.

No comments:

Post a Comment