JOHN TERRY AREJEA CHELSEA, ANTONIO CONTE ATOA NENO - Darajani 1905

JOHN TERRY AREJEA CHELSEA, ANTONIO CONTE ATOA NENO

Share This
Gwiji wa Chelsea, John Terry ambaye kwa sasa anaichezea klabu ya Aston Villa, wiki hii alifika mazoezini na kujumuika kwa pamoja na nyota wa klabu hiyo akikutana pia na kocha wa Chelsea, Antonio Conte ambaye alikuwa naye katika msimu wa mwisho wa gwiji huyo klabuni Chelsea.

Mara baada ya kufika kwenye uwanja huo wa mazoezi wa Cobham Stadium, kocha Antonio Conte alitoa neno juu ya gwiji huyo.

"Alikuwa ni mtu sahihi kuendelea kuwa hapa. Kama ingewezakana angeendelea kubaki klabuni Chelsea. Yeye ni gwiji hapa, na ni mtu muhimu kuwa hapa na naamini anatambua milango ipo wazi kwake muda wote kama atataka kurejea"

"Kiukweli msimu uliopita alikuwa ni mtu wa muhimu kwangu na kwa klabu nzima, alikuwa na sauti kubwa klabuni hapa ingawa hakucheza michezo mingi"

Na alipoulizwa juu ya nini anaona kimepungua mara baada ya gwiji huyo kuondoka Chelsea, kocha Antonio Conte alisema "Alikuwa ni muhimili muhimu na mkubwa kwenye klabu, hakupata nafasi ya kucheza zaidi uwanjani, lakini alikuwa msaada mkubwa kwangu kwenye vyumba vya kubadilishia nguo. Alinifundisha kuongea mambo sahihi kwa muda sahihi" alisema kocha huyo.

Darajani 1905 inaamini pia licha ya gwiji huyo kufika klabuni hapo kama mgeni na kuangalia nini kinaendelea, lakini pia tunaamini alifika hapo kuwapa semina walinzi na nyota wa Chelsea jinsi ya kukabiliana dhidi ya Barcelona katika mchezo wa hatua ya 16 bora ambapo klabu hizo zitacheza usiku wa jumatano huko nchini Hispania.

No comments:

Post a Comment