KINDA WA CHELSEA KAMA HAZARD - Darajani 1905

KINDA WA CHELSEA KAMA HAZARD

Share This
Mara baada ya Eden Hazard kuchaguliwa kuingia kwenye kinyang'anyiro cha kugombania tunzo ya mchezaji bora wa mwezi Februari kwa ligi kuu Uingereza, huko chini napo katika ligi kuu Uingereza kwa vijana, nyota Reece James ambaye anaichezea Chelsea Youth ameingia nae kwenye kinyang'anyiro cha kugombea tunzo ya mchezaji bora wa mwezi Februari kwa ligi kuu Uingereza kwa vijana.

Nyota huyo mwenye miaka 18 ameiongoza vyema klabu ya vijana katika ligi kuu Uingereza kwa vijana akicheza michezo yote ya mwezi huo aliifungia Chelsea goli moja kati ya magoli 4-0 dhidi ya klabu ya vijana ya Manchester united, lakini pia akiisaidia Chelsea katika mchezo wa nusu fainali la kombe la Checkatrade.

Wachezaji anaoshindana nao katika tunzo hizo;
  • Marcus Browne-West Ham
  • Tyrese Campbell-Stoke city
  • Lewis Hardcastle-Birmingham
  • Tahith Chong-Manchester united
  • Lewis Walker-Derby County

No comments:

Post a Comment