CHELSEA YOUTH NAO WASOGEZA MBELE MCHEZO WAO - Darajani 1905

CHELSEA YOUTH NAO WASOGEZA MBELE MCHEZO WAO

Share This
Klabu ya vijana ya Chelsea ya chini ya miaka 18 (Chelsea U18s) ambayo inaongoza msimamo wa ligi kuu chini ya miaka 18 kwa nchini Uingereza ilitakiwa kushuka uwanjani kumenyana  dhidi ya Arsenal U18s ambao wanashika nafasi ya pili katika msiamo huo siku ya tarehe 7-Marchi, lakini mchezo huo umeghairishwa na kuupisha mchezo dhidi ya Leicester city U18s katika kombe la FA ambao wenyewe umepangwa kuchezeka tarehe 6-Marchi mida ya saa 9 mchana.

Mchezo huo ulioghairishwa dhidi ya Arsenal utasogezwa mbele na taarifa juu ya mchezo huo kuchzwa lini nitakuletea zikitoka hapahapa kwenye ukurasa wako maalumu kwa habari za Chelsea kwa lugha yako pendwa ya Kiswahili.

Siku kadhaa zilizopita nilikuletea ripoti juu ya klabu ya wakubwa ya Chelsea kughairisha mchezo wake dhidi ya Burnley, kusoma sababu ya klabu hiyo kughairisha mchezo wake bonyeza hapa


No comments:

Post a Comment