WILLIAN ATOA NENO KUTAKIWA NA REAL MADRID NA BARCELONA - Darajani 1905

WILLIAN ATOA NENO KUTAKIWA NA REAL MADRID NA BARCELONA

Share This
Nyota wa Chelsea, Willian Borges da Silva amekuwa na kiwango kizuri klabuni Chelsea, haswa katika michezo kadhaa iliyopita, akifunga magoli manne katika michezo mitatu. Ambapo amesababisha kuibuka kwa mijadala juu ya kwanini nyota huyo amekuwa haamini sana na kocha wa Chelsea, Antonio Conte ambapo mara nyingi amekuwa akimtumia kama mchezaji wa akiba. Hali inayotajwa kuzipa imani klabu barani Ulaya kuwa wana nafasi kubwa ya kumnasa nyota huyo endapo ikiingia sokoni kumtaka.

Klabu kadhaa kama Manchester united, Ac Milan, Real Madrid na Barcelona zimekuwa zikitajwa kumtaka mbrazili huyo mwenye miaka 29 kwa sasa. Lakini nyota huyo ametoka hadharani na kutoa neno kuhusu kuhusishwa kwake na klabu kadhaa.

"Muda mwengine mchezaji anapoingia kwenye hali fulani mbaya kwake, huwa anataka kuondoka, lakini hiyo sio kwangu. Nipo Chelsea na najiona nipo mahali sahihi na najiona kuwa hapa ndipo pale nilipotamani kuwepo toka mwanzo" alisema nyota huyo.

Kwa kauli hiyo ya mbrazili huyo inaonyesha bado anataka kucheza klabuni hapo na anamapenzi ya dhati kwa klabu hiyo licha ya kutabiriwa mara kadhaa kuwa atakuwa hana maisha marefu klabuni Chelsea kutokana na mara nyingi kutumika kama mchezaji wa akiba. Nasi mashabiki tunafurahi na kupewa nguvu tunaposikia nyota wetu anakuwa na mtazamo chanya kama huu.

No comments:

Post a Comment