Klabu ya Borrusia Dortmund inayoshiriki ligi kuu nchini Ujerumani maarufu kama Bundesliga imekuwa ikimfukuzia nyota wa klabu ya Chelsea mabaye anaichezea klabu yao kwa mkopo, Michy batshuayi mara baada ya nyota huyo mwenye miaka 24 kuwa na kiwango kizuri toka alipofika klabuni hapo kwa mkopo mwezi januari katika dirisha dogo la usajili akifunga magoli matano mpaka sasa.
Mara baada ya kumfukuzia nyota huyo zikatoka taarifa zilizokaririwa kutoka kwa rais wa klabu hiyo akitoa majibu kwamba mmiliki wa klabu ya Chelsea, Roman Abramovich amekataa kumuuza nyota huyo raia wa Ubelgiji.
Kutokana na taarifa hizo vyombo vya habari vikaamua mkumfata nyota huyo na kumhoji juu ya nini anakiwaza mara baada ya muda wake wa kubaki Borrusia Dortmund utakapoisha, ambapo mwisho wa msimu huu ndio atamalizana na klabu hiyo.
"Kwa sasa akili yangu ipo kwenye soka uwanjani, nikishamaliza muda wangu hapa, mwisho wa msimu ndio nitajua kipi cha kufanya kama niendelee kuwa hapa au vipi. Wachezaji wa hapa naelewana nao sana, kuna wanaozungumza kiingereza, kuna wanaozungumza kifaransa na wengine wanazungumza kijerumani, na wote naelewana nao. Hilo ni jambo zuri kwangu" alisema Batshuayi.
Je unadhani atakubali kubaki Dortmund?
BATSHUAYI KUBAKI DORTMUND AU KURUDI CHELSEA?
Share This
Tags
# Majirani
Share This
About Darajani 1905
Majirani
Labels:
Majirani
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment