KUELEKEA MCHEZO WA KESHO, CONTE AMUITA NYOTA MPYA - Darajani 1905

KUELEKEA MCHEZO WA KESHO, CONTE AMUITA NYOTA MPYA

Share This
Kocha Antonio Conte anajiandaa kutua kwenye uwanja wa Etihad kumenyana dhidi ya wenyeji wa uwanja huo, Manchester city katika mchezo wa raundi ya 29 ya ligi kuu Uingereza, huku Chelsea ikihitaji ishinde mchezo huo ili kujipa urahisi katika mbio zake za kupambana kucheza ligi ya mabingwa Ulaya msimu ujao, ambapo inahitaji imalize katika nafasi nne za juu ili kufudhu kucheza michuano hiyo.

Katika safari hiyo, kocha huyo atakuwa pamoja na nyota aliowaita katika kikosi hicho ambapo huenda wakatumika katika mchezo huo. Nyota hao mmojawao ni Josh Grant ambaye hii ni mara ya kwanza kuitwa katika kikosi cha wakubwa akitokea kwenye timu ya vijana ya Chelsea.

Josh Grant mwenye miaka 19 amejumuika pamoja kufanya mazoezi na timu ya wakubwa katika kujiandaa kuelekea kwenye mchezo huo utakaochezwa kesho jumapili saa 7:00.

Nyota huyo anayecheza nafasi ya ulinzi amekuwa na msimu mzuri kwenye timu ya vijana akiisaidia kushinda mataji ya Uefa Youth League kwa msimu wa 2015-2016, kombe la FA kwa vijana misimu ya 2015-2016, na 2016-2017 huku pia akiisaidia kushinda taji la ligi kuu chini ya miaka 18 kwa msimu wa 2016-2017.


No comments:

Post a Comment