HABARI MUHIMU KUELEKEA Man city vs CHELSEA - Darajani 1905

HABARI MUHIMU KUELEKEA Man city vs CHELSEA

Share This
Chelsea leo itakuwa ugenini kucheza mchezo wake wa ligi kuu Uingereza kwa raundi ya 29 ya ligi hiyo ambapo itakuwa kwenye uwanja wa Etihad ili kumenyana dhidi ya Manchester city inayoongoza katika msimamo wa ligi hiyo ikiwa na alama 75. Chelsea inahitaji ushindi katika mchezo huu ili ijiweke sawa katika nia yake ya kumaliza ndani ya nafasi nne za juu katika msimamo huo ili ijiwekee uhakika wa kushiriki michuano ya klabu bingwa barani Ulaya msimu ujao.

Kuelekea kwenye mchezo huo, hapa nakuletea habari muhimu zinazouhusu mchezo huo ambao unatazamwa na wengi kutokana na uhodari wa makocha wa klabu zote mbili.

Habari muhimu;
Chelsea; Kocha Antonio Conte alipofanya mkutano na waandishi wa habari hapo juzi ijumaa alisema nyota watakaokosekana katika mchezo huo ni pamoja na kiungo Tiemoue Bakayoko ambaye amekuwa nje toka mchezo dhidi ya Watford alipopewa kadi mbili za njano zikimaanisha kadi nyekundu huku kukaa kwake nje kukitajwa ni kutokana na majeruhi, David Luiz nae ataendelea kuwa nje pamoja na nyota Ethan Ampadu ambaye alipata majeraha katika mchezo wa ligi ya mabingwa barani Ulaya kwa vijana alipoiongoza vyema klabu ya Chelsea Youth kupata ushindi mnono wa mabao 5-2.

Manchester city; klabu hii itaendelea kuwakosa nyota wake Fernandinho pamoja na Benjamin Mendy ambao wote wanasumbuliwa na majeraha. Lakini pia Kyle Walker na Sterling wanaweza wakaukosa mchezo wa leo

Mwamuzi; Michael Oliver, ndiye mwamuzi wa mchezo huu huku akiwa ndiye mwamuzi mdogo kuliko mwamuzi yoyote pale kwenye ligi kuu Uingereza akiwa na sifa kubwa ya kutoa kadi smbspo mpsks sasa ameshachezesha michezo 30 ya ligi kuu huku akihusika kutoa kadi za njano 109 ambapo kiuiano kila mchezo mmoja anatoa kadi 3 za njano huku katika michezo hiyo akitoa kadi nyekundu.

Rekodi; Katika michezo 108 ambapo Chelsea imekutana dhidi ya Manchester city, Chelsea imeshinda michezo 66 huku ikipoteza michezo 58 na kutoa suluhu michezo 39. Toka mwaka 1993 mpaka mwaka 2009, Chelsea ilipoteza mchezo mmoja tu dhidi ya Manchester city huku Chelsea ikishinda michezo 17 na kutoka suluhu michezo minne.

Michezo iliyopita;
Chelsea; DWLLWL
Manchester city LWWDWW

Muda; Saa 07:00 Usiku (saa 19:00) kwa saa za Afrika Mashariki

No comments:

Post a Comment