"NATAKA MKATABA MPYA" - Darajani 1905

"NATAKA MKATABA MPYA"

Share This

Nyota wa Chelsea, Willian Borges da Silva amekuwa akihusishwa kutakiwa na vilabu kadhaa barani Ulaya huku kocha wake wa zamani aliyewai kumfundisha klabuni Chelsea, Jose Mourinho ambaye kwa sasa anaifundisha klabu ya Manchester united akitajwa kumuwania mbrazili huyo kwa kiasi kikubwa ambapo nyota huyo amekuwa akionekana ana nafasi finyu ya kutumika katika kikosi cha kwanza cha Chelsea iliyochini ya kocha Antonio Conte.

Nyota huyo alifanyiwa mahojiano na chombo kimoja na kusema hatazamii kuondoka Chelsea na kama ikiwezekana yupo radhi aendelee kubaki Chelsea.

"wachezaji wengine wakikutwa kwenye hali kama hii (ya kukosa nafasi katika kikosi cha kwanza) huwa wanafikiria kuondoka, lakini kwangu haipo ivo. Najiona nipo mafanikio nikiwa hapa, najiona nipo mahali sahihi na hata ikiwezekana ninaweza kusaini mkataba mpya ili kuendelea kuwa hapa ata zaidi ya miaka mitano" alisema nyota huyo mwenye miaka 29 kwa sasa.

Nyota huyo amekuwa na kipindi kizuri klabuni Chelsea akiifungia magoli manne katika michezo mitatu iliyopita na leo anatajwa kuiongoza Chelsea kushuka kwenye uwanja wa Etihad kupambana dhidi ya Manchester city.

No comments:

Post a Comment