HAZARD ATOA NENO KUELEKEA MCHEZO DHIDI YA Man City - Darajani 1905

HAZARD ATOA NENO KUELEKEA MCHEZO DHIDI YA Man City

Share This

Wachezaji wa Chelsea wapo jijini Manchester kucheza mchezo wa ligi kuu Uingereza kwa raundi ya 29 leo usiku ambapo Chelsea itakaribishwa kwenye uwanja wa Etihad kumenyana dhidi ya wenyeji wa uwanja huo, Manchester city ambao wenyewe wanaonekana kuwa katika kiwango cha hali ya juu haswa kutokana na kuongoza msimamo wa ligi hiyo kwa alama 75.

Kuelekea kwenye mchezo huo ambao ndio mchezo mzuri zaidi mwisho wa wiki hii kwanza kutokana na ubora wa makocha wa timu hizo ambapo Antonio Conte ameweka historia kubwa kwenye ligi hiyo kwa kubeba taji la ligi hiyo katika msimu wake wa kwanza lakini kwa upande wa Pep Guardiola akionekana kuwa kocha mwenye ubora zaidi msimu huu.

Lakini pia utamu mwengine ukichochewa na ubora wa nyota wa klabu hizo ambapo kwa Chelsea anayetajwa zaidi ni mbelgiji Eden Hazard huku kwa upande w wapinzani akitajwa nyota mwengine mbelgiji, Kevin de Bruyne.

Kuelekea kwenye mchezo huo, nyota wa Chelsea, Eden Hazard ametoa neno kumhusu nyota mwenzake katika timu ya taifa ya Ubelgiji, Kevin de Bruyne.

He doesn't score a lot of goals but he can create something with just one movement or pass. It's simple, he's a special player.

"Ni mchezaji mzuri, anayecheza kwenye klabu bora msimu huu. Ingawa hafungi sana lakini amekuwa na ubora mkubwa"

"City ni timu, timu yenye muunganiko mzuri na kila mchezaji ni mgumu na bora kwenye klabu. Naweza kuiambia timu yangu imzuie De Bruyne au Aguero lakini wapo 11 sio wachezaji wawili tu" alisema nyota huyo ambae amekuwa na akitajwa pia kutakiwa na klabu hiyo ya Manchester city.

Chelsea inahitaji ushindi katika mchezo huu ili ijiwekee nafasi nzuri katika kupambania nafasi ya kucheza ligi ya mabingwa Ulaya msimu ujao.

No comments:

Post a Comment