POLENI WAITALIA NA MASHABIKI WA SOKA - Darajani 1905

POLENI WAITALIA NA MASHABIKI WA SOKA

Share This

Sisi kama mashabiki wa Chelsea, lakini sio wa Chelsea tu bali kama mashabiki wa soka tumehuzunishwa na taarifa za kufariki kwa nahodha wa klabu ya Fiorentina inayoshiriki ligi kuu nchini Italia (Serie A), Davide Astori ambaye amefariki akiwa kwenye chumba cha hoteli nchini humo.

Astori ambaye amefariki akiwa na miaka 31 amefariki kwenye chumba cha hoteli ambapo alikuwa hapo pamoja na timu ya Fiorentina ambayo ilisafiri ili kwenda kucheza mchezo wake wa ligi kuu nchini humo na kifo chake kimekifanya chama cha soka nchini Italia, kughairisha michezo yake ya ligi kuu.

Tunatoa pole kwa familia na watu wa karibu wa nyota huyo raia wa Italia.

No comments:

Post a Comment