ANTONIO CONTE KUONDOKA CHELSEA, GWIJI ATOA NENO - Darajani 1905

ANTONIO CONTE KUONDOKA CHELSEA, GWIJI ATOA NENO

Share This

Mchezo wa leo unatajwa kuwa mchezo muhimu kwa Chelsea kutokana na matokeo ya wapinzani wake katika msimamo wa ligi kuu ambapo jana Liverpool pamoja na Tottenham walipata ushindi na kuongeza pengo la alama kwa Chelsea ambapo Tottenham iliyojuu ya Chelsea kwa sasa ikifikisha pengo la alama tano. Kwa maana hiyo Chelsea inatakiwa ishinde mchezo wake wa leo dhidi ya Manchester city ili kujiweka katika nafasi nzuri.

Lakini pia mchezo huo unatajwa kuwa muhimu kwa kocha Antonio Conte ili kuitetea nafasi yake ya ukocha kwenye klabu ya Chelsea ambapo kama ikitokea Chelsea ikapoteza mchezo wa leo itamaanisha kibarua kitakaribia kuota nyasi kwa kocha huyo.

Kutokana na hali hiyo, gwiji na mkongwe wa soka aliyevuma klabuni Chelsea, Gianfranco Zola ametoa neno kumhusu kocha huyo.

"Ni kweli kuna vilabu vingine wanamsaka Conte kwa karibu lakini Chelsea nayo sio klabu yenye hadhi ndogo. Kwa upande wangu naiona Chelsea kama ni klabu kubwa na yenye hadhi kubwa"

"Kama Chelsea ikimpoteza Conte basi itakuwa imempoteza kocha muhimu na bora na kama Conte akiondoka Chelsea basi atakuwa ameondoka kwenye klabu pekee na bora. Sidhani kama uhusiano wao hauendani, wote wanaendana na wanategemeana"

"Naliongea hilo kwa Chelsea na hata kwa Conte, kama wao wataurekebisha na kuuweka sawa naamini itakuwa ni vyema sana" alisema gwiji huyo ambaye ni raia wa Italia sawa na kocha Antonio Conte.

No comments:

Post a Comment