Mmiliki wa klabu ya Chelsea, Roman Abramovich anatajwa kukubali kumuachia nyota wa klabu yake ya Chelsea, Eden Hazard ili ajiunge na klabu ya nchini Hispania, klabu Real Madrid ambayo imekuwa ikitajwa kumfukuzia winga huyo kwa muda mrefu.
Gazeti la nchini Hispania la Don Balon limetoa taarifa kuwa mmiliki huyo raia wa Urusi anamtaka winga, Gareth Bale wa Real Madrid kama sehemu ya mabadilishano ya usajili wa Eden Hazard ambaye anaripotiwa kutokua tayari kusaini mkataba mpya wa kuendelea kusalia kuwa mchezaji wa Chelsea na sasa Chelsea ipo tayari kumruhusu mchezaji huyo atimkie nchini Hispania lakini tu kama Madrid watakubali kumtumia Bale kama sehwmu ya mabadilishano ya usajili huo.
Chelsea imekuwa ikitajwa kumtaka winga huyo raia wa Wales kwa muda sasa lakini usajili huo umekuwa ukigonga mwamba na sasa usajili huo unaweza kukamilika haswa kutokana na ukubwa wake klabuni Madrid ukionekana kushuka licha ya kusajiliwa kwa dau lililovunja rekodi ya usajili kwa kipindi iko ambapo dau la paundi milioni 85 lilimfanya atue Madrid akitokea Tottenham ya Uingereza.
No comments:
Post a Comment