Chelsea imeshindwa kupata ushindi katika mchezo wa ligi kuu Uingereza mara baada ya kutoka sare ya 1-1 dhidi ya West Ham huku ikiwa nyumbani darajani, Stamford Bridge.
Mara baada ya mchezo huo mlinzi wa Chelsea, Antonio Rudiger amefanyiwa mahojiano na kuulizwa juu ya kilichojiri na kupata sare inayoifanya kuachwa alama 10 huku ikiendelea kuwa kwenye nafasi ya tano ya msimamo wa ligi kuu.
"kiupande wangu hata sijui kipi kiliendelea. mara baada ya kuwa mbele kwa goli 1-0 nashangaa tulikuwa tunapoteza mipira sana na kuwafanya wapinzani kumiliki sana mpira" alisema nyota huyo alipoulizwa anadhani ni nini kiliifanya Chelsea kushindwa kupata ushindi katika mchezo huo wa ligi kuu Uingereza dhidi ya West Ham.
Na alipoulizwa juu ya nini anakifikiria mara baada ya Chelsea kushindwa kupata ushindi ambao ni kama ungemaanisha kutuma salamu za pole kwa gwiji wa Chelsea, Ray Wilkins ambaye alifariki mwanzoni mwa wiki hii, nyota huyo raia wa Ujerumani alisema "ndiyo ni kweli, nina huzuni kwa vile tumeshindwa kumuaga vizuri. Samahani kwa ilo"
"Jambo kubwa ni kwamba tunatakiwa kupambana zaidi na kujitahidi kushinda michezo. Kama tutashindwa kucheza michezo iliyobaki basi itakuwa ngumu kupambania nafasi nne za juu"
No comments:
Post a Comment