Barcelona, Man city kuifata Chelsea fainali klabu bingwa Ulaya - Darajani 1905

Barcelona, Man city kuifata Chelsea fainali klabu bingwa Ulaya

Share This

Klabu ya soka ya vijana chini ya miaka 19 ya Chelsea, Chelsea U19s imefanikiwa kutinga fainali ya klabu bingwa Ulaya kwa vijana (UEFA Youth League) mara baada ya hii leo kuondoka na ushindi wa penati 5-4 mara baada ya dakika tisini kuisha kwa sare ya 2-2 shukrani kwa goli la Josh Grant ambalo alilifunga dakika za majeruhi na kufanya mchezo kuisha kwa sare hiyo ya 2-2 lakini pia shukrani sana kwa mlinda mlango wa Chelsea, Jamie Cumming ambaye alifanya kazi kubwa kwenya matuta akiokoa penati tatu za wapinzani.

Sasa Chelsea U19s imefanikiwa kutinga fainali ya klabu bingwa itakayochezwa siku ya jumatatu ya tarehe 23-Aprili.

Kufanikiwa kwake kushinda katika nusu fainali hiyo mchana wa leo kunamaanisha sasa Chelsea inamsubiri mshindi kati ya Barcelona dhidi ya Manchester city ambao nao wanacheza nusu fainali hii leo ambapo mshindi wa mchezo huo ndio atacheza fainali dhidi ya Chelsea siku hiyo ya jumatatu.

Hongereni vijana wa Chelsea..

No comments:

Post a Comment