Wakati klabu ya Chelsea ilipoutumia mtandao wa Instagram kutuma ujumbe wa kutoa pongezi kwa kikosi cha vijana chini ya miaka 19 cha Chelsea, Chelsea U19s ambao wamefanikiwa kutinga fainali ya klabu bingwa ya vijana (UEFA Youth League) mara baada ya kufanikiwa kuifunga kwa matuta klabu ya vijana ya FC Porto kwa matuta 5-4 mara baada ya muda wa kawaida wa mchezo kuisha kwa sare ya 2-2, nyota wa zamani wa Chelsea raia wa Brazil, Alexander Pato alitoa maoni juu ya ushindi huo katika ujumbe huo wa Chelsea kwa kuandika kikatuni (emoji) ya mkono ukionyesha uimara "💪"
Nyota huyo aliyewai kupita Chelsea kwa mkopo msimu wa 2015-2016 ingawa hakung'aa akiichezea michezo miwili na kuifungia goli moja anaonekana bado ana mapenzi na Chelsea licha ya sasa kuwa nyota wa klabu ya nchini China, klabu ya Tianjin Quanjin ambapo kuendelea kwake kuifatilia (follow) Chelsea katika mitandao ya kijamii kunatafsiriwa ni kutamani kwake kurejea klabuni Chelsea.
Ni nadra kama sio kutokuwepo kabisa kwa nyota kuendelea kuifatilia timu ambayo alipita tena kwa mkopo lakini pia hakung'aa nayo akikosa nafasi na akaendelea kuifatilia. Nyota huyo raia wa Brazil kwa sasa ana miaka 28 na mpaka sasa ameshaichezea klabu yake michezo miwili na kuifungia magoli mawili, usibabaishwe na michezo hiyo michache maana ligi hiyo mpaka sasa ishachezwa michezo 6 wakati mfungaji wao anaeongoza mpaka sasa kwenye timu hiyo ambaye amecheza michezo yote sita, ameshafunga magoli 3 goli moja zaidi ya Pato.
No comments:
Post a Comment