Conte kuwatumia Morata na Giroud, na mengi aliyoyaongea kwenye mkutano hii leo - Darajani 1905

Conte kuwatumia Morata na Giroud, na mengi aliyoyaongea kwenye mkutano hii leo

Share This

Chelsea itacheza mchezo wake wa nusu fainali ya kombe la FA siku ya jumapili ya tarehe 22-Aprili pale kwenye uwanja wa Wembley uliopo jijini London dhidi ya Southampton, klabu inayofundishwa na nyota wa zamani wa Chelsea, Mark Hughes.

Kuelekea kwenye mchezo huo muhimu kwa Chelsea ambapo ni muhimu kushinda ili kuwa na matumaini ya kushinda taji kwa msimu huu ambapo hili ndio taji pekee ililobakiza kwa msimu huu kati ya mataji manne iliyoshiriki toka mwanzoni mwa msimu.

Kocha Antonio Conte amefanya mkutano na waandishi wa habari mchana wa leo akihojiwa juu ya mchezo huo unaofata wa nusu fainali ya kombe hilo la FA.

Alianza kwa kuulizwa juu ya nini anakiongea kuhusu kocha wa Arsenal, Arsene Wenger ambaye ametangaza kustaafu ukocha ifikapo mwishoni mwa msimu huu huku akidumu katika fani hiyo kwa takribani miaka 22 akiifundisha klabu hiyo ya Arsenal, kocha Antonio Conte alijibu akisema hiyo ni taarifa ya huzuni maana kocha huyo amekua bora huku akiwa na uwezo mkubwa wa kuifundisha timu kwa umakini na ustadi mkubwa.

Lakini pia akasema anadhani kocha huyo ameacha historia kubwa kwenye alama ya soka ambapo anaamini ni ngumu kwa kocha wa sasa kuweza kudumu na timu moja kwa muda mrefu kama kocha huyo.

Alipoulizwa juu ya kutumia washambuliaji wawili Olivier Giroud pamoja na Alvaro Morata kwenye mchezo uliopita dhidi ya Burnley, kocha huyo alisema hii ni mara ya kwanza kuwatumia washambuliaji wawili ambao kiasili ni namba tisa kwenye mchezo mmoja kwa Chelsea ingawa kwenye klabu alizowai kuzifundisha zote alikuwa akitumia mfumo huo wa washambuliaji wawili ambapo alisema faida ya kutumia washambuliaji wawili ni pamoja na kuweza kulishambulia lango la mpinzani kwa pamoja ni tofauti na kumtumia mshambuliaji mmoja ambae anapata upinzani kutoka kwa walinzi wengi kwenye eneo la hatari la wapinzani.

Lakini pia hakusita kufafanua juu ya tukio la mshambuliaji wa Chelsea, Alvaro Morata ambapo alionekana akikasirika mara baada ya kufanyiwa mabadiliko katika mchezo wa dhidi ya Burnley na nafasi yake kuchukuliwa na Eden Hazard ambapo kocha alisema nyota huyo alikasirika kutokana na kukosa goli la wazi kwenye mchezo huo na sio kama ilivyozaniwa na wengi kuwa mchezaji huyo hakupenda kutolewa.

Kwa kumalizia kocha huyo aliulizwa juu ya kiwango cha Emerson Palmieri na Tiemoue Bakayoko ambao wote aliwaongelea kwa maelezo ya kufanana akisema wote ni wachezaji wenye umri mdogo na wenye uwezo mkubwa huku akionyesha kufurahishwa na kiwango alichokionyesha Bakayoko kwenye mchezo dhidi ya Burnley.

Swali la mwisho ambalo ni kama lilikuwa la utani ni pale alipoulizwa kuhusu kuzima simu yake mara baada ya mkutano uliopita simu kupigwa kuita akiwa katikati ya mkutano ambapo alilazimika kuizima huku akiomba msamaha na kusema mkewe ndie aliekuwa akimpigia ambapo kwenye mkutano wa leo alionyesha kuwa simu yake ameizima huku akisema hawezi kurudia kosa maana yeye sio mpumbavu.

No comments:

Post a Comment