Tanzia; Chelsea yakumbwa na msiba mwengine - Darajani 1905

Tanzia; Chelsea yakumbwa na msiba mwengine

Share This

Hizi ni taarifa mbaya na za huzuni kwa klabu na mashabiki wa Chelsea duniani kote.

Gwiji na mchezaji wa zamani wa Chelsea, Roy Bentley amefariki dunia akiwa na miaka 93 huko nchini Uingereza. Bentley aliyewai kutamba na kikosi cha Chelsea akiwa kwenye kikosi bora kilichoshinda ubingwa wa ligi daraja la kwanza mwaka 1955 huku akiwa mfungaji bora wa ligi katika misimu saba tofauti akiichezea Chelsea jumla ya michezo 367 huku akiifungia magoli 150 amefariki dunia hii leo huku akiwa bado na mapenzi makubwa na Chelsea huku akihudhuria michezo kadhaa ambayo Chelsea imecheza Stamford Bridge.

Bentley ambaye pia alikuwepo uwanjani wakati Chelsea ilipotwaa taji la ligi kuu Uingereza mwaka 2005 akiwa sambamba na nahodha John Terry ambapo siku hiyo ilikuwa ikitimia miaka 50 toka kulibeba taji hilo pindi alipokuwa mchezaji mwaka 1955.

Jambo ambalo huenda hulijiui kuhusu hayati marehemu huyu ni kwamba dau la paundi 11,000 ndilo lilimfanya akatua Chelsea ingawa sababu kubwa iliyomfanya akatua Chelsea ni kutokana na ushauri aliopewa na daktari kuwa kutokana na matatizo aliyokuwa nayo ya mapafu basi itabidi ajiunge na klabu inayopatikana kwenye nyanda za kusini ambapo huko ndiko ilipo klabu ya Chelsea ambayo yenyewe inapatikana magharibi-kusini.

Msiba huu unakuja baada ya wiki kadhaa zilizopita Chelsea ilipokumbwa na msiba wa gwiji mwengine wa klabu hiyo, Ray Wilkins.

Roho ya marehemu ilazwe mahali pema peponi, Amen.

No comments:

Post a Comment