Klabu ya vijana wenye umri chini ya miaka 19, Chelsea U19s inafanikiwa kupata ushindi wa muhimu unaoifanya kufudhu kucheza fainali za klabu bingwa barani Ulaya mara baada ya kupata ushindi wa matuta wa 5-4 dhidi ya FC Porto mara baada ya dakika tisini kuisha kwa sare ya 2-2.
Mchezo huo uliochezwa huko jijini Nyon nchini Switzerland ambao ulikuwa mchezo wa nusu fainali na kama unavyojua michuano hii ya vijana haina marudiano na huenda ndio maana ukachezwa Switzerland iwe kinyume na mahali zinapotokea klabu hizo ambapo Chelsea ni ya Uingereza wakati FC Porto ni ya Ureno kwa maana hiyo mchezo huu ilikuwa ni lazima mshindi apatikane na kufudhu kucheza fainali ya michuano hiyo kwa vijana chini ya miaka 19.
Alikuwa ni yuleyule nyota wa Chelsea ambaye ameonyesha kiwango cha hali ya juu kwenye michuano hii, Redan ambaye ndie alikuwa wa kwanza kufungua pazia la ufungaji akifunga goli jepesi ambapo goli hilo liliifanya Chelsea iamini inaweza ikamaliza kipindi cha kwanza ikiwa inaongoza mpaka pale hali ipokua mbaya mara baada ya goli hilo kusawazishwa na kufanya mchezo kwenda mapumziko huku matokeo yakiwa 1-1.
Kipindi cha pili kilianza huku kila timu ikijitahidi kutengeneza mashambulizi na ndipo wakati ziliposalia dakika kumi mchezo kuisha FC Porto wakafanikiwa kupata goli la pili na kuifanya Chelsea kupoteza matumaini ya kucheza fainali lakini mwisho wa siku shujaa akabaki kuwa shujaa mara baada ya nahodha Josh Grant kuchomoa goli hilo na kufanya mchezo kuwa 2-2 na mpira kuisha huku wakiwa wametoshana nguvu.
Kutokana na kanuni za mashindano, ikaamriwa kupigwe matuta ambapo huko shujaa aliibuka mlinda mlango wa Chelsea, Jamie Cumming ambapo kwa uwezo wake mkubwa wa kuokoa penati tatu ukaifanya Chelsea U19s iondoke na ushindi wa matuta 5-4.
No comments:
Post a Comment