Dakika ya 71' mwamuzi msaidizi wa mchezo wa Burnley dhidi ya Chelsea alionyesha ubao wenye namba 9 yenye rangi nyekundu na namba 10 yenye rangi ya kijani ambapo ubao huo ulimaanisha mabadiliko yalikuwa yakifanyika kwa upande wa Chelsea ambapo mshambuliaji wa Chelsea, Alvaro Morata ilitakiwa atoke na nafasi yake kuchukuliwa na winga Eden Hazard, wakati huo Chelsea ilikuwa tayari inaongoza kwa magoli 1-2.
Lakini wakati Morata akiwa anatoka na kufika kwenye benchi la Chelsea alionekana kukasirika na kutokua na furaha kabisa huku wengi wakitafsiri kukasirika kwake kule ni kutokana na kutopendezwa na maamuzi ya kupumzishwa wakati mwenyewe alitamani kuendelea lakini pia ikitafsiriwa kuwa kocha Antonio Conte aliamua kumpumzisha kutokana na goli la kizembe alilokosa ambalo lingeweza kuifanya Chelsea kuongoza kwa magoli mawili lakini akakosa goli hilo lakini dakika kadhaa baadae Burnley wakasawazisha na kufanya mchezo kulingana kwa magoli 1-1 mpaka pale Victor Moses alipoifungia Chelsea goli la ushindi na kufanya matokeo kuwa 1-2.
Nyota huyo raia wa Hispania ametumia mtandao wa Instagram akituma ujumbe wa kueleza kufurahishwa na ushindi huo wa jana maana una maana kubwa katika kujiandaa kucheza mchezo wa nusu fainali ya kombe la FA dhidi ya Southampton, mchezo utakaochezwa siku ya jumapili pale kwenye uwanja wa Wembley.
Lakini pia nyota huyo akatumia mtandao huo kuwaelewesha watu na mashabiki wa soka juu ya kushangazwa kwao kwa kitendo cha nyota huyo kukasirika wakati alipotolewa ambapo mwenyewe alisema kukasirika kwake sio kutokana na kutolewa au kupumzishwa ila alikasirika kutokana na kuumizwa na goli alilokosa kwenye mchezo huo.
Nyota huyo ameshaichezea Chelsea michezo 42 na kuifungia magoli 14 tangu asajiliwe na Chelsea akitokea Real Madrid kwa dau la paundi milioni 60.
Kusoma alichoshauriwa na kocha Antonio Conte, bonyeza hapa
No comments:
Post a Comment