Klabu ya vijana ya Chelsea ambayo ilifanikiwa kuitupa nje klabu ya vijana ya Real Madrid kwenye michuano ya klabu bingwa barani Ulaya kwa wachezaji vijana wenye umri chini ya miaka 19 kwenye mchezo wa robo fainali, klabu ya Chelsea U19s inatarajia kushuka uwanjani mchana wa leo kucheza mchezo wake wa nusu fainali ya michuano hiyo ya klabu bingwa ikicheza dhidi ya FC Porto.
Jijini Nyon nchini Switzerland ndipo kutakapochezwa mchezo huo wa nusu fainali huku nyota wa Chelsea, Ethan Ampadu atakuwa nje akiukosa mchezo huu kutokana na majeraha aliyoyapata kwenye mchezo wa robo fainali dhidi ya Real Madrid ambapo Chelsea U19s iliondoka na ushindi wa magoli 2-5.
Kama Chelsea ikifanikiwa kupata ushindi kwenye mchezo huo wa leo basi itafanikiwa kucheza fainali ya michuano hiyo.
No comments:
Post a Comment