Chelsea yamfata tena kiungo wa PSG - Darajani 1905

Chelsea yamfata tena kiungo wa PSG

Share This

Chombo cha habari cha nchini Ufaransa ambacho kimekuwa kikiaminika juu ya taarifa zake za usajili, RMC Sport kimeripoti Chelsea inaifukuzia saini ya kiungo na nyota wa PSG ambaye ni raia wa Argentina, Javier Pastore ambaye anaonekana kutohitajika kwenye kikosi hicho cha PSG.

Nyota huyo ambaye aliwai kutakiwa kwa karibu na Chelsea ameingia kwenye orodha ya wachezaji wanaotaka kuachwa na kikosi hicho kutokana na sheria za usajili za kuagiza klabu isajili na kuuza kwa kiwango cha pesa kinachoendana.

Nyota huyo ana mkataba na klabu hiyo unaoisha mwezi Juni mwaka 2019 na inaelezwa klabu yake ya PSG haitokuwa tayari kumuachia aondoke bure kwenye kikosi chao.

No comments:

Post a Comment