Chelsea inapata ushindi wa magoli 1-2 ikiwa ugenini ikicheza dhidi ya Burnley katika mchezo wa ligi kuu Uingereza ambapo mchezo huo ulichezwa kwenye uwanja wa Burnley, uwanja wa Turf Moor na kufanikiwa kuondoka na alama zote tatu kwa ushindi huo ambao magoli yake yalichangiwa kwa kiasi kikubwa na winga wa Chelsea, Victor Moses aliyefunga goli la ushindi huku goli la kwanza akiwa amesababisha mlinzi wa Burnley ajifunge.
Lakini Chelsea ingeweza kujihakikishia ushindi mapema kama sio kosa lililofanywa na mshambuliaji wa Chelsea, Alvaro Morata aliyekosa goli la wazi kabisa akibakia yeye na mlinda mlango wa Burnley, Pope.
Mara baada ya kosa hilo, kocha Antonio Conte alihojiwa mwishoni mwa mchezo juu ya kuamua kumtoa mhispania huyo huku nafasi yake ikichukuliwa na Eden Hazard kwamba je kocha aliamua kumtoa kutokana na kukosa kwake goli hilo la wazi? kocha Antonio Conte akajibu akisema "Hapana, nilihitaji kuingiza nguvu mpya ili akaongeze nguvu mpya" lakini pia alipoulizwa juu ya mfumo alioanza nao katika mchezo huo kwa kuwaanzisha washambuliaji wa kati Olivier Giroud na Alvaro Morata.
"Nadhani wanaendana wakicheza pamoja, lakini kwa nafasi ambazo Morata amekua akizikosa inabidi apate hasira na kupambana ili awe sawa" alisema kocha huyo.
 
 
 
  
 
 
 
 
 
 
No comments:
Post a Comment