Nyota wa Chelsea, Hannah Blundell anafanikiwa kusaini mkataba mpya wa kuwa mchezaji wa klabu ya wanawake ya Chelsea, Chelsea Ladies.
Blundell ambaye amekua akicheza kama winga anayecheza pia kama mlinzi wa pembeni (wing-back) amekuwa muhimili mkubwa kwenye kikosi cha Chelsea Ladies tangu alipoichezea mchezo wa kwanza mwaka 2013 huku akifanikiwa kuichezea kwa mara ya kwanza kikosi cha timu ya Uingereza huku akiwa mchezaji wa Chelsea.
"Kiukweli nimekuwa mwenye furaha sana, haswa nilipopewa taarifa kwa klabu kua wanataka nisaini mkataba mpya. Hapa ni kama nyumbani na najiona niko pamoja na familia kuwa sehemu kama hii."
"Namshukuru pia kocha wangu Emma Hayes kwa kunisaidia kuanzia ndani ya uwanja mpaka nje ya uwanja" alisema nyota huyo ambaye kwa sasa ana miaka 23.
Lakini pia nyota huyo amefanikiwa kuingia kwenye kikosi bora cha ligi kuu ya wanawake nchini Uingereza inayotolewa na chama cha wanasoka wakulipwa (PFA Team of the year) akiwa sambamba na wachezaji wenzake wa Chelsea Ladies ambao ni Ji So-Yun, Millie Bright, Fran Kirby, Maren Mjelde pamoja na mwenyewe Hannah Blendell.
 
 
 
  
 
 
 
 
 
 
No comments:
Post a Comment