Moses aibuka shujaa, Burnley 1-2 Chelsea - Darajani 1905

Moses aibuka shujaa, Burnley 1-2 Chelsea

Share This

Ni usiku mwengine mtamu kwetu mashabiki wa Chelsea duniani kote mara baada ya usiku wa leo kupata ushindi katika mchezo wa muhimu dhidi ya Burnley kwa magoli 1-2.

Jitihada kubwa ikifanywa na Victor Moses hatimaye mchezaji wa Burnley akajifunga na kuifanya Chelsea kuwa mbele kwa goli 0-1 mpaka mchezo kwenda mapumziko.

Kipindi cha pili kilianza na Barnes wa Burnley akasawazisha na kufanya mchezo kuwa sare ya 1-1 mpaka pale Victor Moses alipoifungia Chelsea goli la pili na la ushindi unaoifanya Chelsea ifufue matumaini yake ya kushiriki michuano ya klabu bingwa barani Ulaya kwa msimu ujao.

Lakini ukiachana na uwezo mkubwa ulioonyeshwa na Victor Moses katika ushindi huu muhimu lakini pia nyota mwengine wa Chelsea, Emerson Palmieri ameonyesha umahiri wa hali ya juu mara baada ya kuonyesha kwa kiasi gani Chelsea itafaidi makubwa kutoka kwake ambaye usiku wa leo ndio ameichezea Chelsea mchezo wa kwanza wa ligi kuu Uingereza huku akihusika kwa kutoa pasi ya mwisho iliyoipa Chelsea goli la ushindi lililofungwa na Victor Moses.

No comments:

Post a Comment