Chelsea inatajwa kuachana na kocha wake wa sasa, Antonio Conte mara baada ya kocha huyo kutokua na msimu mzuri mpaka sasa ambapo katika michuano minne ambayo Chelsea imeshiriki ni michuano ya kombe la FA tu pekee inayoonekana kuwa na nafasi ya kuitwaa ikiwa ipo katika hatua ya nusu fainali ambapo itacheza dhidi ya Southampton.
Lakini kuachana kwa kocha huyo inamaanisha klabu hiyo itataka kuingia sokoni ili kumsaka kocha mpya atakayeweza kuziba pengo la kocha huyo raia wa Italia ambaye amebakiza mkataba wa mwaka mmoja na miezi miwili wa kuendelea kusalia kama kocha wa Chelsea.
Maurizzio Sarri, kocha wa Napoli anatajwa tena kutakiwa na Chelsea mara baada ya hapo mwanzo kuhusishwa kutakiwa na Chelsea kabla ya rais wa klabu yake kutangaza kufanya mazungumzo na kocha huyo ili asaini mkataba mpya wa kuwa kocha wa klabu hiyo.
Lakini kocha huyo ametajwa tena na baadhi ya vyombo vya habari kuwa mrithi wa kocha Antonio Conte klabuni Chelsea huku dau la paundi milioni 7 likitajwa kama dau la kuweza kumng'oa kwenye klabu hiyo ya nchini Italia inayoshiriki ligi kuu nchini humo.
No comments:
Post a Comment