Usiku huu klabu ya vijana ya Chelsea ya chini ya miaka 18 inashuka uwanjani Stamford Bridge kucheza mchezo wa marudiano dhidi ya Birmingham City katika hatua ya nusu fainali.
Mchezo huu ni mchezo wa pili wa nusu fainali ambapo mchezo wa kwanza ambao Chelsea ilikuwa ugenini kwenye uwanja wa St. Andrews Stadium, Chelsea ilifanikiwa kupata ushindi mnono wa magoli 0-3, magoli yakifungwa na Tariq Uwakwe, Charlie Brown na Callum Hudson-Odoi na kuifanya Chelsea iliyochini ya kocha Jody Morris kuwa na faida ya magoli matatu ya ugenini.
Chelsea inaingia kwenye mchezo huu huku ikiwa na faida hiyo ya magoli matatu huku ikiwa na rekodi nono ya kutokupoteza mchezo wowote ikiwa nyumbani katika michezo 55.
Nitakuletea habari zote juu ya kilichojiri kwenye nusu fainali hii.
No comments:
Post a Comment