Chelsea itakuwa uwanjani jioni ya leo ikicheza dhidi ya West Ham katika mchezo wa ligi kuu Uingereza kwenye uwanja wa Stamford Bridge.
Kuelekea kwenye mchezo huo, hapa nakuletea habari muhimu za kuelekea kwenye mchezo huo wa ligi kuu Uingereza kwa mchezo wa 32 kwa upande wa Chelsea huku timu nyengine zikiwa zimeshacheza michezo 33.
Habari muhimu;
Chelsea; Kurejea kwa Thibaut Courtois, Ross Barkley, Danny Drinkwater na Pedro Rodriguez kunaweza kumfanya kocha Antonio Conte awe na uwanja mpana wa kuweza kuchagua wachezaji watakaoweza kutumika kwenye mchezo huu wa leo ambao Chelsea inahitaji ipate ushindi ili kujiweka sawa kwenye msimamo wa ligi kuu.
Kylian Hazard ambaye ni mdogo wake na Hazard anaweza pia kutumika kwenye mchezo wa leo mara baada ya kujumuishwa kwenye mazoezi ya kikosi cha kwanza cha Chelsea kwa wiki nzima wakati Chelsea ikiwa inajiandaa. David Luiz na Ethan Ampadu nao bado hawajawa sawa kurejea uwanjani.
West Ham; Michael Antonio na Manuel Lanzini wote wataukosa mchezo wa leo kutokana na majeraha huku wengine watakaokua nje ni pamoja na James Collins, Winston Reid, Pedro Obiang, Sam Byram na Andy Carroll ambao wote wanasumbuliwa na majeruhi.
Mwamuzi; Kevin Friend, ana miaka 46 kwa sasa huku akiwa amekuwa mwamuzi katika michezo 28 huku akitoa kadi za njano 58 huku akitoa kadi nyekundu 1 kwa msimu huu wa 2017-2018.
Rekodi; Chelsea haijawai kupoteza michezo mfululizo ikiwa Darajani [Stamford Bridge] dhidi ya timu za jiji la London toka ilipotokea mara ya mwisho mwaka 1999.
Michezo iliyopita;
Chelsea; LLWLL
West Ham; WLLLW
Muda; Saa 06:30 Jioni (Saa 18:30) Kwa saa za Afrika Mashariki
No comments:
Post a Comment