John Terry atamba kwenye kikosi bora, aweka rekodi - Darajani 1905

John Terry atamba kwenye kikosi bora, aweka rekodi

Share This

Mchezaji wa zamani wa Chelsea ambaye alikuwa nyota na nahodha mkubwa klabuni hapo, John Terry ambaye kwa sasa ana miaka 37 akiwa anaitumikia klabu ya Aston Villa kwa sasa amefanikiwa kuingia kwenye kikosi bora cha mwaka kwa ligi daraja la kwanza nchini Uingereza akiwa na klabu hiyo ya Aston Villa.

John Terry alijiunga na klabu hiyo mwaka 2017 mara baada ya kuachwa na Chelsea ambapo angeweza kujiunga na klabu inayoshiriki ligi kuu lakini mwenyewe alikataa kulifanya hilo akikataa kucheza dhidi ya klabu yake ya Chelsea ambapo amefanya hivyo tofauti na alivyofanya Frank Lampard ambaye alikubali kujiunga na Manchester city.

Mpaka sasa ameshaichezea Aston Villa michezo 31 kati ya michezo 41 huku akiwa ametengeneza muimala mkuu kwenye safu ya ulinzi na kuisaidia vyema katika mbio zake za kutaka kurejea ligi kuu Uingereza.

John Terry pia alitimiza mchezo wa 800 mwisho wa wiki iliyopita, akiweka rekodi ya kuwa moja ya wachezaji waliocheza michezo mingi nchini Uingereza.

Kikosi kamili cha michuano hiyo;
John Ruddy (Wolves)
Ryan Fredericks (Fulham)
Ryan Sessegnon (Fulham)
Conor Coady (Wolves)
John Terry (Aston Villa)
Tom Cairney (Fulham)
Ruben Neves (Wolves)
James Maddison (Norwich City)
Bobby Reid (Bristol City)
Albert Adomah (Aston Villa)
Matej Vydra (Derby County)

Kocha: Neil Warnock (Cardiff City)

No comments:

Post a Comment