Magoli 14 kwenye michezo 40 ya michuano yote huku akionekana hana msimu mzuri mpaka sasa ingawa alianza kwa kasi kubwa akifunga magoli nane kwenye michezo nane ya mwanzo. Ni Alvaro Morata raia wa Hispania, amefunguka kwanini hana msimu mzuri mpaka sasa licha ya kuanza akiwa kwenye ubora wa hali ya juu.
"Kila kitu kilikuwa sawa mpaka pale nilipopata matatizo ya mgongo. Nilijilazimisha kucheza huku nikiwa na maumivu nadhani ingekua sahihi na vyema kama ningeamua kupumzika. Lakini niliona itakuwa vyema nikiendelea kucheza na wenzangu kwa ajili ya timu na mashabiki. Lakini sasa hayo yamepita"
"Mwaka wangu wa kwanza ungeweza kuwa mzuri, lakini kuna michezo mingi bado na tuna nafasi ya kushinda kombe la FA" alisema mshambuliaji huyo.
Morata alisajiliwa na Chelsea kwa paundi milioni 60 akitokea Real Madrid na tangu ametua Chelsea amekuwa akitumika kama mshambuliaji nambari moja kwenye kikosi kilichochini ya kocha Antonio Conte ambacho kinapambania nafasi ya kumaliza katika nafasi nne za juu ili kuweza kufudhu kucheza klabu bingwa barani Ulaya kwa msimu ujao lakini pia kikiwa na nafasi ya kushinda taji la kombe la FA ikiwa hatua ya nusu fainali dhidi ya Southampton siku ya tarehe 22-Aprili.
No comments:
Post a Comment