Alisajiliwa akitokea klabu ya nchini kwao Ufaransa, klabu ya St. Etienne na kutua Chelsea kwa dau la paundi milioni 12 na kusaini mkataba wa miaka mitano na nusu na akionyesha kiwango cha hali ya juu kabla ya kupata majeraha katika mchezo dhidi ya Man utd hiyo ilikuwa mwaka 2016 na alikaa nje kwa miezi sita.
Alianza kufanya mazoezi klabuni Chelsea na baadae kusaini mkataba mpya wa miaka sita, hiyo ikiwa katika dirisha kubwa la usajili la mwaka 2017 ambapo pia alipata fursa ya kujiunga kwa mkopo na klabu ya Stoke city.
Kurt Zouma, kijana mwenye miaka 23 huku akiwa ameshaichezea kwa mkopo klabu ya Stoke city michezo 33 mpaka sasa huku akiwa mlinzi imara kwenye safu ya ulinzi ya klabu hiyo ambayo haionekani kuwa na msimu mzuri mpaka kufikia sasa.
Nyota huyo atarejea Chelsea na kuungana na kikosi hicho mwishoni mwa msimu huu ambapo ndio muda mkataba wake wa mkopo na klabu hiyo utakuwa unamalizika.
Mchezaji mkongwe raia wa Uingereza, Peter Crouch ambaye ni mshambuliaji wa klabu hiyo ametoa neno juu ya ubora wa nyota huyo raia wa Ufaransa "Kuisaidia Stoke hilo ndicho kipaumbele chake, hiyo ilianza toka alipofika hapa kwa mara ya kwanza. Ni kawaida kwa wachezaji wa mkopo kujitenga na timu pindi inapokuwa kwenye wakati mgumu lakini Kurt (Zouma) amekuwa kiongozi kwa kila hatua"
"Amekuwa mchezaji mzuri na nimeshashiwishika nae na naamini atakuwa chaguo la kwanza klabuni Chelsea na hata timu ya taifa ya Ufaransa. Ana sifa zote kama mlinzi makini, mlinzi mwenye nguvu na mpambanaji" alisema mkongwe huyo.
No comments:
Post a Comment