Batshuayi kuwai kurejea uwanjani - Darajani 1905

Batshuayi kuwai kurejea uwanjani

Share This
Nyota wa Chelsea, Michy Batshuayi ambaye kwa sasa ana mkataba wa mkopo na klabu ya Borrusia Dortmund ambayo amejiunga nayo katika dirisha dogo la usajili la mwezi Januari ambapo mkopo klabuni huko ulikuwa unaisha mwezi Juni alipata majeraha kwenye mchezo wa ligi kuu Ujerumani dhidi ya Schalke 04 ambapo Dortmund ilipoteza kwa mabao 2-0 ikiwa ugenini alipopata majeraha kwenye mchezo huo alikimbizwa hospitalini ambapo baadae majibu yalikuja yakisema amevunjika kifundo cha mguu na hatorejea uwanjani katika kipindi chote cha msimu uliobaki.
Nyota huyo raia wa Ubelgiji ametuma ujumbe wa picha kupitia mtandao wa Instagram akionyesha jinsi alivyoimalika na kuonesha maendeleo aliyokuwa nayo kwa sasa.
Nyota huyo ambaye mara baada ya kufanyiwa matibabu na kuanza kutembelea kwa msaada wa magongo ametuma video hiyo huku akiambatanisha na maneno akisema anazidi kuimalika na kuzidi kuwa imara.
Mpaka kupata majeraha yake hayo ameshaichezea klabu hiyo ya nchini Ujerumani michezo 14 na kuifungia magoli 9 na alipatwa na kadhia hiyo siku ya tarehe 16-Aprili, mpaka kufikia hii leo zimepita siku tano toka nyota huyo apatwe na majanga hayo.

No comments:

Post a Comment