Kocha wa zamani wa Barcelona ambaye aliwai kutakiwa na Chelsea kabla ya klabu hiyo kumnasa kocha wake wa sasa Antonio Conte, kocha Pep Guardiola ambaye kwa sasa anaifundisha klabu ya Manchester city ameitaja klabu ya Chelsea kuwa ndio imekataa matumizi ya teknolojia ya Video-Assistant Referee (VAR) ambayo hutumia marudiano ya tukio lililotokea kwa kuonyesha kwenye video ambapo hiyo humsaidia mwamuzi kurudia tukio ambalo hana uhakika nalo na kutoa maamuzi sahihi.
Kocha huyo alipohojiwa alisema "(Manchester) City walikubali kutumika kwa teknolojia hiyo lakini klabu za juu kwenye msimamo wa ligi kuu zilizokataa mfumo huo kutumika nadhani ni Chelsea na Man utd." alisema kocha huyo
"Ujue mpira siku hizi umekuwa wa kasi sana, waamuzi wanahitaji kupata wasaidizi kabla ya kufanya maamuzi. Mpaka leo hatujui penati aliyopewa Madrid dhidi ya Juventus kama ilikuwa ya halali ama sio" alimalizia kocha huyo raia wa Hispania.
Kulifanyika upigwaji wa kura ulioendeshwa kwa makocha na viongozi wa klabu za Uingereza ili kuupigia kura mfumo huo kama utumike au usitumike msimu ujao wa ligi kuu Uingereza ambapo baadae ikaonekana klabu hizo hazijawa tayari kuutumia mfumo huo na hivyo kukataliwa. Mfumo huo utatumika pia kwenye michezo ya fainali za kombe la dunia mwaka huu uko nchini Urusi.
Mfumo huo pia umekuwa ukilalamikiwa na mashabiki wengi wa soka lakini pia na kundi kubwa la wanaohusika na mchezo huo wakidai unapoteza radha ya mpira huku wengi wakikerwa na usimamaji wa mchezo ili mwamuzi aweze kupokea majibu juu ya marudio ya tukio ambayo hufanyiwa usahihi kwenye chumba cha waamuzi ambao wao ndio wanalikariri tukio hilo kisha kumpa majibu mwamuzi.
No comments:
Post a Comment