Gwiji wa Chelsea, Frank Lampard ameteuliwa rasmi kuwa kocha wa klabu ya Derby County inayoshiriki ligi daraja la kwanza nchini Uingereza maarufu kama Championship.
Lampard amechaguliwa kuwa kocha wa klabu hiyo huku msaidizi wake akiwa ni Jody Morris ambaye alikuwa mchezaji wa zamani wa Chelsea lakini pia amekuwa akiifundisha klabu ya vijana wenye umri chini ya miaka 18 wa Chelsea ambao msimu huu wameshinda mataji manne.
Lampard ambaye amepewa mkataba wa miaka mitatu kuifundisha klabu hiyo amesema " Mara zote nimekuwa natamani kuiongoza klabu yenye historia na hazina kubwa kama Derby County, kwa hiyo hii ni nafasi kubwa na ya muhimu kwangu. Nimetumia muda mwingi kujadiliana na kupanga mipango mingi pamoja na viongozi wa klabu pamoja na mwenyekiti"
"Tuna lengo la kumaliza kwenye nafasi sita za juu kwenye msimamo wa Championship kama ilivyofanya msimu ulioisha, tutawatumia wachezaji makinda na waliokuwepo hapa Pride Park"
"Hii ni kazi yangu ya kwanza kama kocha, lakini nimeshafanya kazi na kuwa karibu na makocha wengi bora na najiamini mimi mwenyewe pamoja na wanaonizunguka, ikiwemo bodi ya timu. Najua haitokua kazi rahisi kufundisha timu kama hii ila natazama mbele kuelekea kwenye mafanikio" alisema gwiji huyo aliyecheza Chelsea kwa miaka 13 huku akishinda mataji mengi na kuweka rekodi kibao.
Hongera kwake...
No comments:
Post a Comment