Rasmi; Chelsea yazitangaza jezi za msimu wa 2018-2019 - Darajani 1905

Rasmi; Chelsea yazitangaza jezi za msimu wa 2018-2019

Share This

Sasa ni michezo miwili imebaki ili msimu wa 2017-2018 umalizike ambapo Chelsea itacheza dhidi ya Newcastle katika mchezo wa ligi kuu Uingereza na dhidi ya Manchester united katika fainali ya kombe la FA. Ni kama msimu umemalizika.

Hii inamaanisha Chelsea inajiandaa kuingia msimu mpya, msimu wa 2018-2019 na ili kulionyesha hilo klabu ya Chelsea FC imezindua fulana (jersey) ambazo itazitumia kama fulana zake maalumu (home kit) ambapo wamezizindua kupitia mtandao wa Twitter.

Fulana hizo zitatumika kama fulana maalumu (home kit) kwa timu zote zilizochini ya Chelsea ambazo ni Chelsea FC, Chelsea Ladies (klabu ya soka ya wanawake) na Chelsea Youth (klabu zote za vijana kwenye akademi) kwa msimu wote wa 2018-2019.

No comments:

Post a Comment