Mashabiki wa Chelsea wamtaka gwiji wa Chelsea arithi mikoba ya Antonio Conte - Darajani 1905

Mashabiki wa Chelsea wamtaka gwiji wa Chelsea arithi mikoba ya Antonio Conte

Share This

Hakuonekani kuwa na matumaini ya kocha Antonio Conte kuendelea kusalia klabuni Chelsea haswa kama akishindwa kuisaidia klabu hiyo kufudhu kucheza michuano ya klabu bingwa barani Ulaya kwa msimu ujao  ambapo mpaka sasa ili Chelsea ifudhu kucheza michuano hiyo ya klabu bingwa inahitaji Liverpool ipoteze mchezo wa mwisho huku Chelsea ni lazima iondoke na ushindi. Lakini pia sababu kubwa ikitajwa kushindwa kuelewana na bodi ya Chelsea ambayo amekua akiilalamikia juu ya mfumo wa usajili.

Lakini sasa mashabiki wa Chelsea wametumia mtandao wa Twitter kutuma ujumbe kuonyesha wanahitaji kama kocha huyo raia wa Italia akiachana na Chelsea basi nafasi yake ichukuliwe na mchezaji wa zamani wa klabu hiyo, Jody Morris ambaye kwa sasa ni kocha wa kikosi cha vijana cha Chelsea kwa wenye umri chini ya miaka 18 maarufu kama Chelsea U18.

Kocha huyo raia wa Uingereza amekiongoza vyema kikosi hicho cha vijana kushinda mataji manne huku ikishindwa kulitwaa taji moja tu la klabu bingwa barani Ulaya ambapo ilicheza fainali ya michuano hiyo na kupoteza mbele ya Barcelona, fainali ilichezwa jijini Nyon huko Switzerland.

Kocha huyo alituma ujumbe kwenye mtandao wa Twitter akiwashukuru mashabiki na wapenzi wa Chelsea walioonyesha kuwashangilia kwenye mchezo wa ligi kuu kati ya Chelsea dhidi ya Huddersfield ambapo yeye pamoja na kikosi cha vijana hao walifika uwanjani kutoa shukrani kwa mashabiki wa Chelsea huku wakiyatambulisha mataji hayo manne waliyoyashinda msimu huu.

Ndipo ujumbe huo ukapokelewa na mashabiki wengi wa Chelsea ambapo wengi wao walikua wakimuuliza ni lini kocha huyo atarithi mikoba ya Antonio Conte na kuwa kocha wa kikosi cha wakubwa. Lakini pia huku wengine wakitoa maoni kwa kusema kocha huyo anastahili kabisa kuwa kocha wa kikosi cha Chelsea FC

No comments:

Post a Comment