Heri ya kuzaliwa 'Mikono 1000', je unajua kwanini anataka kwenda Madrid? - Darajani 1905

Heri ya kuzaliwa 'Mikono 1000', je unajua kwanini anataka kwenda Madrid?

Share This

Leo ni siku muhimu kwa mlinda mlango wa Chelsea, Thibaut Courtois au unaweza kumuita Mikono 1000 ambapo siku kama ya leo yaani tarehe 11-May mwaka 1992 alizaliwa rasmi huko jijini Bree nchini Ubelgiji.

Lakini leo sitaki nikuletee mbwembwe na maneno mengii kuhusu siku muhimu ya mlinda mlango huyu mwenye ulukuki wa mataji na tunzo binafsi alizowai kuzishinda na anazoendelea kuzishinda mpaka pale atakapoamua rasmi kutundika glavu zake na kuitwa gwiji.

Leo nataka nikupe mambo matatu ambayo labda huyajui na hata kama unayajua basi blog yako ya Darajani 1905 inataka ikujuze zaidi.

1. Kwanza tuanze na familia yake, je unajua kama familia ya nyota huyu ilikuwa haipo kwenye masuala ya soka? wazazi na dada wa nyota huyu wote walikua wachezaji wa mchezo wa mpira wa mkono (Volleyball) na nyota huyu alishaanza kufuata mkondo mpaka pale alipofikisha miaka 12 alipoamua kuingia kabisa kwenye mchezo wa soka.

2. Mwaka 2013, moja ya mashabiki wa soka nchini Colombia aligundua neno la "Thibauting" ambalo lilionyesha mapenzi yake kwa mlinda mlango huyo lakini neno hilo lilionekana kupendezwa na wengi mpaka kufikia hatua likapewa heshima nchini kwao Ubelgiji. Neno hilo lilichaguliwa kuwa neno bora la michezo kwa mwaka huo.

3. Nadhani umekua ukifuatilia kauli za nyota huyo ambapo aliwai kutoa kauli akisema moyo wake upo Hispania, kama unakumbukumbu vizuri kauli hiyo ilizua utata mkubwa ikihusishwa kua anatamani kujiunga na Real Madrid lakini baadae nyota huyo alikuja na kusema alisema vile kutokana na familia yake kuishi nchini  humo. Lakini bado mimi nawewe tulibaki na maswali, kwanini familia yake isihamishiwe nchini Uingereza ili aungane nayo? Sasa leo nitakupa jibu kamili kwanini familia hiyo isiungane nae nchini Uingereza!

Ipo hivi, nyota huyo alipofika nchini Hispania ili kuichezea klabu ya Atletico Madrid kwa mkopo alikutana na mchumba raia wa nchini, Marta Dominguez humo na kufanikiwa kupata watoto wawili lakini baadae akatengana na mwanamke huyo na ikabidi mwanamke huyo abaki na watoto kutokana na sheria zinavyoamuru.

Kurejea kwa nyota huyo nchini Uingereza ili kuichezea Chelsea kukamaanisha watoto wa nyota huyo kusalia na mama yao nchini Hispania na ndio maana Courtois akasema moyo wake upo kwenye jiji la Madrid kutokana na watoto wake kuishi jijini humo nchini Hispania.

Hongera Mikono 1000 kwa kutimiza miaka 26.

No comments:

Post a Comment