Bayern Munich watua kwa winga wa Chelsea - Darajani 1905

Bayern Munich watua kwa winga wa Chelsea

Share This

Klabu ya Bayern Munich inayopatikana nchini Ujerumani inatajwa na gazeti la Kicker la nchini humo kumfatilia mlinzi na winga wa kushoto wa klabuni Chelsea anayeichezea kwa mkopo klabu ya Newcastle ya nchini Uingereza, Kenedy Robert.

Gazeti hilo la Kicker linaitaja klabu hiyo kuwa kwenye mpango wa kumtafuta mlinzi wa kushoto kuwa mbadala wa Julian Bernat na inatajwa kumtazamia Kenedy kuwa chaguo sahihi kutokana na makubwa aliyoyaonyesha klabuni Newcastle ambapo alijiunga napo katika dirisha dogo la usajili la mwezi Januari.

Lakini pia klabu ya Newcastle inatajwa kumuwania nyota huyo ili imsajili kwa usajili wa moja kwa moja huku ikisubiri majibu kutoka kwa kocha wa Newcastle, Rafa Benitez ambaye alishawai kuifundisha klabu ya Chelsea alishawai kudai anapendezwa na nyota huyo na atashinikiza kufanyike mazungumzo ili nyota huyo atue Newcastle.

No comments:

Post a Comment