Ripoti kamili kuhusu tunzo za Chelsea - Darajani 1905

Ripoti kamili kuhusu tunzo za Chelsea

Share This

Usiku wa kuamkia leo tarehe 11-May mwaka 2018 huko jijini London nchini Uingereza kumefanyika shughuli maalumu ikiihusisha klabu ya Chelsea FC ambayo inaambatana na klabu kwa soka la wanawake maarufu kama Chelsea Ladies ambayo huutumia uwanja wa Kingsmeadow kama uwanja wake wa nyumbani lakini pia ikiziongoza klabu za vijana zinazotofautiana na umri ambazo hutajwa kwa mjumuisho kama Chelsea Youth ambapo ndani yake kuna klabu za vijana zinazotenganishwa kwa umri.

Katika shughuli hiyo ya utolewaji wa tunzo kwa wachezaji waliofanya vizuri kwa msimu mzima wa 2017-2018 na hivi ndivyo tunzo zilivyotolewa.

Tunzo ya goli bora la msimu; Willian Borges da Silva
Tunzo ya mchezaji bora kwa akademi ya vijana (Chelsea Youth); Reece James
Tunzo ya mchezaji bora kwa wachezaji wenzake kwa klabu ya wanawake (Chelsea Ladies); Fran Kirby
Tunzo ya mchezaji bora wa mwaka kwa wanawake (Chelsea Ladies); Fran Kirby
Tunzo ya mchezaji bora chipukizi; Andreas Christensen
Mchezaji bora kwa upande wa mdhamini wa Chelsea, Yokohama Tyres; N'Golo Kante
Tunzo ya mchezaji bora kwa wachezaji wa Chelsea FC; Willian Borges da Silva
Tunzo ya mchezaji bora wa mwaka; N'Golo Kante

Utabiri wangu ulienda sawa kwa Willian Borges ambaye goli lake dhidi ya Brighton & Hove ambalo lilifungwa likitengenezwa na kupikwa na Eden Hazard pamoja na Michy Batshuayi ndilo limechaguliwa kuwa goli bora la mwaka ambapo kama kumbukumbu zako zitakuwa vizuri goli hilo lilishinda pia kwenye tunzo ya goli bora la mwezi Januari kwa ligi kuu Uingereza.

Utabiri wangu mwengine nilitabiri N'Golo Kante kushinda tunzo ya mchezaji bora kwa wachezaji ambapo tunzo hiyo imenaswa na Willian Borges huku Kante akichaguliwa kuwa mchezaji bora wa mwaka.

Hongereni nyota wetu.

No comments:

Post a Comment