Tunzo za Chelsea usiku wa leo - Darajani 1905

Usiku huu kunafanyika shughuli kubwa na ya muhimu pale klabuni Chelsea ambapo kunafanyika tafrija ya utolewaji wa tunzo kwa wachezaji ndani ya klabu zilizochini ya klabu ya Chelsea FC ambazo ni Chelsea FC yenyewe, Chelsea Ladies maalumu kwa soka la wanawake na Chelsea Youth maalumu kwa vijana wa akademi.

Tunzo hizo ambazo ni maalumu kwa wachezaji na wote waliofanya vizuri kwa msimu mzima wa 2017-2018 inatolewa usiku wa leo na kama ilivyoada blog yako pendwa ya Darajani 1905 itakuletea washindi wa tunzo hizo kwa msimu huu.

Baadhi ya tunzo zinashoshindaniwa ni pamoja na goli bora la msimu, mchezaji bora wa msimu ambayo msimu uliopita alishinda Eden Hazard pamoja na tunzo ya mchezaji bora kwa wachezaji ambayo msimu uliopita alishinda N'Golo Kante.

Utabiri wangu kwa msimu huu;
Tunzo ya mchezaji bora wa mwaka atashinda Cesar Azpilicueta ambaye nami nilimpigia kura wakati tunzo ya mchezaji bora kwa wachezaji anaweza akashinda N'Golo Kante wakati kwa upande wa goli bora anaweza akashinda Willian Borges ambalo goli lake dhidi ya Brighton lililoshinda goli bora la mwezi.

No comments:

Post a Comment