Klabu ya Chelsea inaweza kupigwa rungu na chama cha soka cha nchini Uingereza mara baada ya kutolewa ripoti na chama hicho maarufu kama FA
Ripoti iliyotolewa leo hii kutoka kwenye chama hicho kinadai klabu ya Chelsea inaingia kwenye mashtaka kutokana na kosa lililofanywa na wachezaji pamoja na watu wa benchi la ufundi kwa kumzingira mwamuzi, Lee Mason katika mchezo wa jana kati ya Chelsea ilipocheza dhidi ya Huddersfield, mchezo ulioisha kwa sare ya 1-1.
Tukio lililoifanya Chelsea iingie kwenye mashtaka hayo lilitokea pale mwamuzi Lee Mason alipopuliza filimbi ya kumaanisha ni muda wa mapumziko wakati mchezaji wa Chelsea alipokua anajiandaa kupiga kona jambo ambalo liliwakera wachezaji pamoja na makocha wa Chelsea ambapo walivamia uwanja na kuanza kumzonga mwamuzi huyo wakihoji kwanini mchezo ulimalizwa muda ambao Chelsea ilitakiwa ipige mpira wa kona. Wakati huo matokeo yalikuwa 0-0 na Chelsea ilihitaji ushindi ili ijiweke sawa kwenye mbio za kumaliza kwenye klabu nne za juu za kushiriki klabu bingwa msimu ujao.
Chama hicho cha FA kimetoa ripoti hiyo na kuagiza Chelsea kama itakuwa na cha kujitetea katika hilo basi ifike kwenye ofisi za chama hicho siku ya jumanne ya tarehe 15-May mwaka huu.
No comments:
Post a Comment