Winga na nyota wa Chelsea, Eden Hazard amekua akihusishwa kutimkia klabuni Real Madrid kwa muda mrefu huku kocha wa klabu hiyo ya nchini Hispania, Zinedine Zidane akitajwa kuwa ndiye mtu anayechochea kwa kiasi kikubwa usajili huo kutimia ingawa rais wa klabu hiyo, Fiorentino Perez anatajwa kutomhitaji sana winga huyo raia wa Ubelgiji.
Mchambuzi wa chombo cha habari za michezo cha Sky Sports, Tony Cottee ambaye aliwai kuwa mchezaji wa klabu ya West Ham anadai nyota huyo ataondoka au kusalia klabuni Chelsea endapo akipata ufumbuzi kwa jambo moja tu.
Mchambuzi huyo anadai winga huyo mwenye miaka 27 ambaye amebakiza miaka miwili kwenye mkataba wake wa klabuni Chelsea ataondoka klabuni hapo au kusalia na kusaini mkataba mpya ambao klabu yake ya Chelsea imekuwa ikijaribu kumshawishi endapo nyota huyo atajua kama klabu hiyo itamuajiri kocha mwengine au itaendelea kusalia na kocha wa sasa Antonio Conte.
Klabu ya Chelsea imekua ikitajwa kumsaka kocha mpya wa kurithi nafasi ya kocha Antonio Conte ingawa taarifa hizo hazina uthibitisho wa moja kwa moja haswa kutokana na kocha huyo kukiri hana mpango wa kuondoka klabuni hapo huku akiwa bado ana mkataba wa mwaka mmoja wa kuendelea kuinoa Chelsea.
No comments:
Post a Comment