Nyota wa klabu ya Chelsea, Alvaro Morata amekua akihusishwa kutakiwa na klabu ya Juventus ya nchini Italia ambapo anatajwa kutakiwa na klabu hiyo ili akawe mrithi wa mshambuliaji wa klabu hiyo, Mario Mandzukic ambaye anatajwa kuachana na klabu hiyo mwishoni mwa msimu huu.
Lakini kuondoka kwa Morata kunatajwa kuifanya Chelsea kuanza taratibu za kumfukuzia mshambuliaji wa klabu ya Ufaransa, Edinson Cavani ambaye ni raia wa Uruguay huku akiwa na rekodi ya kuwa mfungaji bora wa muda wote klabuni hapo.
Nyota huyo mwenye miaka 31 kwasasa ametoa majibu ya kuhusishwa kwake kutakiwa kuondoka kwenye klabu hiyo ambao ni mabingwa wa ligi kuu nchini Ufaransa kwa maarufu kama Ligue 1. Mshambuliaji huyo amedai hana mpango wa kuondoka klabuni hapo na ana mipango ya muda mrefu klabuni hapo.
No comments:
Post a Comment