Chelsea Ladies yakaribia ubingwa ligi kuu Uingereza - Darajani 1905

Chelsea Ladies yakaribia ubingwa ligi kuu Uingereza

Share This

Klabu ya soka ya wanawake ya Chelsea maarufu kama Chelsea Ladies kimefanikiwa kupata ushindi mwengine ikiwa nyumbani kwenye uwanja wake wa nyumbani, Kingsmeadow dhidi ya Birmingham kwa magoli 2-1 na kufanikiwa kurejea kileleni mwa msimamo wa ligi kuu ya wanawake nchini Uingereza.

Chelsea ilianza kupata goli lake la kwanza kupitia kwa nyota wake Fran Kirby na kuifanya klabu hiyo kuongoza mpaka pale Birmingham waliposawazisha na kufanya matokeo kuwa sare ya 1-1 lakini wakati mpira ukielekea kuisha nyota wake ambaye ni kinda wa miaka 17, Erin Cuthbert akafanikiwa kuifungia Chelsea goli la pili na la ushindi klabu yake hiyo.

Ushindi huo unaifanya Chelsea Ladies kufikisha alama 35 ambazo zinaifanya kuwa kileleni mwa ligi hiyo huku ikifukuziwa kwa karibu na Manchester city. Chelsea imebakiza michezo mitatu ambayo kama ikishinda inakuwa bingwa wa michuano hiyo.

No comments:

Post a Comment