Batshuayi kicheko, Hazard majanga kuelekea Kombe la Dunia - Darajani 1905

Batshuayi kicheko, Hazard majanga kuelekea Kombe la Dunia

Share This

Sasa kila utakapopita habari ni moja tu, kuhusu Kombe la Dunia. Kila mtu anazungumzia Kombe la Dunia litakalofanyika huko nchini Urusi na limebakiza siku tatu tu kabla ya kuanza kutimua vumbi.

Ubelgiji ni moja ya timu zinazotegemewa kufanya makubwa kwenye michuano hiyo haswa kutokana na ubora wa kikosi chake na aina ya wachezaji iliyobarikiwa timu hiyo kutoka barani Ulaya. Lakini timu hiyo ndiyo imekuwa timu ya mwisho shiriki ya michuano hiyo kucheza mchezo wake wa mwisho wa kujiandaa na michuano hiyo hapo jana wakicheza dhidi ya timu yenzake shiriki kwenye michuano hiyo, Costa Rica.

Na kama unavyojua Ubelgiji ina nyota watatu wa Chelsea ambao ni Eden Hazard, Michy Batshuayi pamoja na Thibaut Courtois ambao wote walipata nafasi ya kucheza kwenye mchezo huo lakini Batshuayi akiingia kama mchezaji wa akiba katika dakika ya 52' akichukua nafasi ya Dries Mertens.

Mchezo huo ulianza kwa nyota wa zamani wa klabu ya Fulham, Bryan Ruiz kuifungia goli la kwanza Costa Rica katika dakika ya 24' lakini Ubelgiji wakasawazisha kupitia kwa Dries Mertens kabla ya kuongeza tena mawili kupitia kwa Romelu Lukaku na goli la nne likifungwa na Michy Batshuayi na kukamilisha ushindi mnono wa magoli 4-1.

Lakini wakati mchezo ukiwa unaelekea mwishoni, dakika ya 70' nyota wa Chelsea, Eden Hazard alitoka kwa majeraha hali iliyowafanya wengi kuwa na wasiwasi kama atakuwa sawasawa kucheza michuano hiyo.

Punde nitakuletea alichokisema kocha wake wa Ubelgiji, Roberto Martinez nini amekisema juu ya maumivu hayo ya nyota huyo.

No comments:

Post a Comment