Heri ya kuzaliwa Zappacosta na mwenzako, unajua mwenzake ni nani? - Darajani 1905

Heri ya kuzaliwa Zappacosta na mwenzako, unajua mwenzake ni nani?

Share This

Leo ni siku ya pekee kwa nyota wawili wa Chelsea ingawa wengi wamemtazama nyota mmoja tu, Davide Zappacosta kwa kumtakia heri ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwake. Lakini Darajani 1905 tunamtakia pia heri kinda wa Chelsea anayetamba na kikosi cha vijana wenye umri chini ya miaka 18 cha Chelsea (Chelsea U18s), Billy Gilmour.

Leo ni siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwa wawili hawa ambapo Zappacosta anatimiza miaka 26 wakati Gilmour anatimiza miaka 17 toka kuzaliwa kwake mwaka 2011.

Kutokana na takwimu za mtandao wa Wikipedia unaelezwa kwamba tangu Zappacosta atue Chelsea mwaka 2017 akitokea Torino ya Italia amefanikiwa kuichezea timu hiyo michezo 22 na kuifungia goli moja alilolifunga kwenye mchezo wa klabu bingwa barani Ulaya dhidi ya AS Roma na ameisaidia Chelsea haswa kwenye nafasi ya winga na mlinzi wa kulia akitumika kama mbadala wa Victor Moses.

Kwa upande wa Billy Gilmour, huyu anatajwa kama moja ya wachezaji wenye vipaji vya hali ya juu kutokea nchini Scotland ambapo alianza maisha ya soka katika akademi ya Rangers kabla ya kusajiliwa na Chelsea mwaka 2017 akiwa bado ana miaka 15 lakini alipotimiza miaka 16 mwaka huo alisaini mkataba mpya na Chelsea kama mchezaji wa hadhi ya juu (professional footballer) na sasa anatamba na kikosi hicho cha vijana cha Chelsea na amekuwa mmoja wa nyota waliopita kwenye mafanikio ya kocha aliyejiunga na Derby County kama kocha msaidizi wa Lampard, Jody Morris wakati kikosi hicho cha vijana kiliposhinda mataji manne kati ya matano huku ilo taji la tano wakilipoteza kwenye fainali.

Hongereni nyota wetu...

No comments:

Post a Comment